Kamanda muriro amesema;
“Katika kuelekea mchezo huo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam litachukua tahadhari zote za kiusalama kabla, wakati na baada ya mchezo, usalama utaimarishwa kwa kiwango cha juu”
“Ni marufuku kwa Mtu yeyote kwenda na silaha uwanjani isipokuwa vyombo vya dola vyenye jukumu la usalama eneo hilo, tunawatoa hofu Mashabiki watakaofika kushuhudia mchezo huo kuwa ulinzi ndani na nje ya uwanja utakuwa umeimarishwa kwa kiwango cha juu”
Mechi hiyo itakua ni mechi ya ufunguzi wa msimu wa 2022/23 utakaopigwa kesho August 13 2022 uwanja Benjamin mkapa